Thursday, August 11, 2011
Mahojiano ya Mwandishi Nova Kambota na Askofu Sylvester Gamanywa!
1.Baba Askofu umewahi kunukuliwa ukisema “gharama ya kuilinda amani iliyopo ni ndogo kuliko gharama ya kuirudisha amani ikishapotea” je kimsingi una maana gani baba Askofu ?
JIBU
Maana yangu ilikuwa ni kuitahadharisha jamii itafakari kwa kina kuhusu matokeo ya kuvunjika kwa amani. Hakuna uamuzi usiokuwa na gharama. Uamuzi wa kuivunja amani una matokeo kinyume na kuwepo kwa amani yenyewe. Matokeo hayo kinyume ni pamoja na kupanda kwa gharama za maisha, kwa sababu uzalishaji pamoja na huduma za kijamii zinazotolewa wakati wa amani vitakoma, na jamii italazimika kujitafutia njia mbadala za kujikimu ambazo zitakuwa ni ngumu na aghali sana.
Hapo sizungumuzii suala la kuongezeka kwa majeruhi wa vita na machafuko ambayo wahusika pamoja na kuachishwa uzalishaji; lakini watahitaji tiba ambazo ama hazitakuwepo kabisa, au zikiwepo zitakuwa ni aghali hazinunuliki, matokeo yake ni wengi kupoteza maisha au kuwa na vilema vya maisha.
Si hayo peke yake, hata juhudi za kujaribu kuirejesha amani iliyotoweka nako kutagharimu zaidi. Maana itatuchukua muda mrefu zaidi kuirejesha. Isitoshe, wapo wengine ambao hawatakubali amani irejee kwa sababu tu wananufaika na mazingira ya vita na machafuko.
Sasa basi, kwa mwananchi wa kawaida ambaye mpaka hivi, katika mazingira ya utulivu bado maisha yake ni shida tupu; je! hali yake ya maisha itakuwaje pale ambapo gharama za maisha zitapanda ghafla na kudumu kwa muda usiojulikana wa kutokuwepo kwa amani? Nilitaka jamii ilitafakari hili.
2. Uhuru wa vyombo vya habari unaongeza uelewa miongoni mwa wananchi na pia unachochea tabia na mienendo ya wananchi kiasi kwamba kumeibuka hali ya vuta nikuvute baina ya viongozi na wananchi, je unaliongeleaje hili? Unadhani ni kweli kuna uhuru wa habari? Una manufaa gani?
JIBU
Kuna tofauti kati ya kuwa na “uhuru wa habari” na “matumizi sahihi ya uhuru wa habari”. Tukifanya tathmini kuanzi miaka 20 iliyopita, (kwa sisi tulioshuhudia mwanzo wa uhuru, azimio la Arusha mpaka Azimio la Zanzibar), hakuna wa kubisha kwamba Tanzania tunao uhuru wa habari. Hata kama uhuru wenyewe sio asilimia mia moja, lakini upo tena unaotushinda hata kule kuutumia ipasavyo.
Tatizo kubwa tena linaloelekea kuwa sugu ni dalili za kuwepo kwa “matumizi yasiyo sahihi ya uhuru wa habari”. Bila shaka, tatizo hili linachangiwa kwa kiasi kikubwa na mazingira mapya ya utandawazi, uchanga wa uwezo wa umilikaji wa vyombo vya habari pamoja na ukiukwaji wa maadili ya habari.
Kwa hiyo, kile kinachoonekana kuwa ni “hali ya vuta nikuvute baina ya viongozi na wananchi” hakikusababishwa na kuwepo kwa uhuru wa habari bali matumizi yasiyo sahihi ya uhuru wa habari.
3. Wewe kama mmoja wa wadau wa maadili kwenye taifa, je umelipokeaje swala la baadhi ya wabunge kutaka kupigana bungeni? Na una ushauri gani?
JIBU
Kwanza, bado tunapaswa kukumbuka kwamba demokrasia yetu bado ni changa. Pili, kwa mujibu wa taratibu za kuwapata viongozi wa kutuwakilisha katika ngazi za udiwani, ubunge hata urais, maadili kama maadili katika maana yake halisi bado si kigezo kinachopewa uzito unaostahili. Tafuta mwenyewe uone sifa za mtu kugombea nafasi ya uongozi katika ngazi husika, sifa ya maadili haimo.
Kwa hiyo, si ajabu kama kutajitokeza dalili za ukiukwaji wa maadili katika Nyanja za uongozi. Ni vema tukumbuke kwamba mlango wa kukiukwa kwa maadili umeachwa wazi tangu awali kwenye sifa za kuwapata viongozi katika ngazi husika. Hapa itabidi tusubili ujio wa katiba mpya pengine tutapata ufumbuzi wakati huo ukifika. Nikiwa na maana kwamba kigezo cha maadili kama mojawapo ya sifa ya kupata viongozi kitazingatiwa kikamilifu.
4.Rushwa umekuwa ni mwiba sasa kwa taifa letu licha ya kazi za TAKUKURU na sheria zilizopo, je nini nafasi ya viongozi wa dini katika kupambana na rushwa?
JIBU
Hili ni swali zito na muhimu. Siwezi kulijibu kwa haraka na kwa ufupi katika jukwaa lako. Linahitaji mjadala mzito, tena wa kuwahusisha kikamilifu viongozi wa dini. Nasema hivi kwa sababu rushwa sio tu kuwekewa TAKUKURU na sheria za nchi, lakini pia imeandikwa katika misahafu ya dini zetu.
Nafasi pekee ya viongozi wa dini, katika kupambana na rushwa, ni kurejea upya maagizo na sheria zilizomo katika misahafu ya dini husika. Kipaumbele kisiwe kukomea katika kukemea rushwa katika jamii, badala yake uzito mkubwa uelekezwe katika kurejesha maadili ya kiimani ambapo rushwa inatafsiriwa kuwa ni dhambi mbaya na hatari hivyo lazima iogopwe.
Kila mwamini aelimishwe bayana kwamba adhabu ya Mwenyezi Mungu kwa dhambi ya rushwa ni Jehanamu ya moto. Pasipo mtu kuwa na hofu ya Mungu siku ya kiyama hakuna silaha itakayofaulu katika kudhibiti rushwa.
5. Kumekuwa na tuhuma za baadhi ya viongozi wa dini kutumiwa na wanasiasa nchini kufanikisha malengo yao, je wewe kwa upande wako limewahi kukukuta? Na je ni kweli lipo hili au ni uzushi tu?
JIBU
Mimi nami nimezisikia kama wewe. Kwa kumbukumbu zangu binafsi zijawahi “Kutumiwa na siwezi kutumiwa” na wanasiasa kwa malengo yao. Kila mahali popote niliposhirikiana na viongozi wa kisiasa chimbuko lake ni ubunifu wangu na ushawishi wangu kwao na kunipa fursa ya kutimiza malengo ya wito wangu kwa Mungu na kwa taifa. Siwezi kuwasemea wengine katika hili sababu sina ushahidi wala uthibitisho.
6. Matumizi ya mabavu dhidi ya wananchi hususani kutoka kwa vyombo vya usalama limekuwa ni tatizo siku za karibuni, je wewe kama kiongozi wa kiroho na mwananchi unaliongeleaje hili?
JIBU
Tatizo la msingi katika hili haliko kwenye vyombo vya usalama wala jamii. Tatizo liko kwenye mfumo uliopo wa mahusiano kati ya pande husika. Mfumo huu unaweza kurekebishwa vizuri pale ndoto za katiba mpya zitakapotimia.
7. Rais wa Jamhuri ya Muungano amewataka viongozi wa dini kujiepusha na biashara haramu ya madawa ya kulevya tena ameonya kuwa baadhi ya viongozi wa dini wanajihusisha na biashara hii haramu na baadhi ya viongozi wa dini wakaja juu wakimtaka athibitishe madai yake kwa kuwataja wahusika, je! wewe unalipokeaje hili?
JIBU
Hili nimelipokea kama bomu ambalo limelipukia kwenye kambi ya madhehebu ya dini. Hii ni kashfa nzito. Aliyeiweka hadharani ni mtu mzito, mkuu wa nchi mwenye vyombo vya dola. Wenzangu wamesema lakini mimi bado natafakari kwanza. Nasali kwa Mungu anipe ufunuo wa lipi niseme, niseme kwa nani na ili iweje.
8. Tiba ya Loliondo imekuwa ni moja kati ya mambo yaliyovuta hisia za viongozi wa dini huku baadhi wakipinga na wengine wakiunga mkono, je wewe kama mmoja wa viongozi wa dini unaliongeleaje hili? Na upi msimamo wako katika tiba ya Loliondo?
JIBU
Tangu habari hizi zianze kupewa uzito wa pekee na vyombo vya habari, kila nilipohojiwa jibu langu lilikuwa moja, “nafanya utafiti”. Kusema kweli mpaka sasa bado nafanya utafiti. Utafiti ninaoufanya ni kujua kwa hakika kwa kupitia maandiko matakatifu ya Biblia kama bado Mungu anatoa mafunuo na maagizo ya tiba kupitia dawa, vitambaa, maji ya Baraka, nk. Nikikamilisha utafiti wangu nitasema wakati huo. Msimamo wangu utajengwa kwenye taarifa ya utafiti ninaofanya hivi sasa.
9. Mihadhara ya kidini imekuwa sio tena sehemu ya kufundishana dini bali kukashfiana na pole pole uvumilivu wa kidini umeanza kutoweka, je unadhani kuna haja ya kupiga marufuku mihadhara ya kidini?
JIBU
Nani apige marufuku na kwa mamlaka ya nani? Je! Huu si ndio uhuru wa kuabudu na kueneza imani kwa mujibu wa haki za binadamu? Haya ni maswali yanayogongana akili mwangu lakini si majibu ya swali lako. Majibu ni kwamba, katiba mpya ndio ufumbuzi wa hii mitafaruku ya kidini ambayo inaonekana kuwa kero.
Unaweza kucheka kila ninapojibu kwa kutaja hoja ya “katiba mpya”. Lakini nina maana kamili katika kujibu hivi. Nami nimejiandaa kushiriki kikamilifu na uzito wangu utajikita katika nafasi ya “Haki na Uhuru wa kuabudu na kueneza dini; pamoja na mahusiano yanayotakiwa kuwepo “kikatiba” kati ya dini na serikali.
10. Mwisho kabisa baba kwenye changamoto lukuki kama maandamano ya CHADEMA, ugumu wa maisha, malumbani ya wanasiasa, migomo ya vyuo vikuu na ajali za barabarani za mara kwa mara zinazolikumba taifa letu nini mtazamo wako, maoni na ushauri wako kwa viongozi wa dini, serikali na jamii kwa jumla?
JIBU
Majibu yangu, mtazamo wangu, na ushauri wangu kwa viongozi wa dini, serikali na jamii kwa jumla ni kuwa na “katiba mpya”! Asante sana mhariri.
Sunday, August 7, 2011
JOHN LISU BAADA YA AFLEO AJA NA KITU KIPYA
JMUIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI TANZANIA JOHN LISU ALIYEFANIKIWA KUTEKA NYOYO ZA WATU WENGI NDANI YA NCHI NA NJE YA NCHI AMETANGAZA KUJA NA KITU KIPYA KWA MWAKA 2O11 AKIHOJIWA KUPITA KITUO CHA MATANGAZO YA RADIO CHA PRAISE POWER CHA JIJINI DAR ES SALAM KUPITIA KIPINDI CHA SIFA MOTO JOHN LISU ALISEMA SAFALI HII AMEAMUA KUFANYA CONCERT YA JEHOVA YU HAI TOUR 2011 NA AKASEMA HUU NI MWANZO TU LAKINI AMEWATAKA WAPENZI WAKE WOTE WALIOKO MIKOANI WAKAE MKAO WA KURA KWANI MAMBO NDIO KWANZA YAMEANZA BLOG HII INAMTAKIA JOHN LISU MAFANIKIO MEMA KATIKA KUHIHUBIRI INJIRI YA KRISTO AMEN
WAIMBAJI WA EBENEZER MINISTRY (EMT) WAPATA ULAJI
WINNER MAGELE |
LUCY CHALAMILA
EDWIN OTEN
JOYCE MHINGA a.k.a MAMA GODLOVE
Saturday, May 21, 2011
TALAJIA KUPATA MAMBO MEMA
Mpendwa wangu wewe ambaye ni shabiki wa blog yangu tarajia kupata mambo mema na mazuri kupitia blog ya http://www.magele.blogsport.com/ siku si nyingi Mungu akubariki kila unapotembelea blog hii kikubwa zaidi ni kuniombea ili Mungu azidi kunipa vitu vizuri vya kukuelimisha wewe mpenzi msomaji wangu ili uzidi kukuwa kimwili na kiroho.
Sunday, May 15, 2011
HIVI NDIVYO MAZISHI YA WAIMBAJI WAWILI WA AMBASSADORS HUKO RWANDAYALIVYOKUWA
Waliokuwa waimbaji wa Ambassadors of Christ waliolala mauti Amosi,Philbert na Gatare Jim Ephraim
Waimbaji wa Ambassadors wakiwa wamebeba jeneza
Mke wa Gatare Jim Ephraim akilia
Umati wa watu ndani ya Kanisa la Waadventista Wasabato Remera wakati wa ibada ya mazishi
Baba wa Gatare Jim Ephraim akizungumza |
Mama wa Gatare Jim Ephraim
Matukio ya Ajali iliyoleta Majonzi Kwenye Kundi la Kwaya La Ambassadors Of Christ!
Baadhi ya umati uliojitokeza kusubiria majeruhi na miili ya marehemu
Ndugu ,jamaa na marafiki wakiwa hospitali
Baadhi ya ndugu na jamaa na marafiki wakiwa nje ya hospitali
Helcopter iliyobeba majeruhi pamoja na miili ya marehemu
Helcopter hiyo iliyokuwa imebeba miili ya marehemu pamoja na majeruhi ikitua
Baadhi ya majeruhi wakishushwa kutoka kwenye helcopter
Ndugu na jamaa wakiwa nje ya hospitali
Baadhi ya ndugu na jamaa wakiwa katika hali ya majonzi na masikitiko makubwa
BLOG HII INAWAPA POLE NDUGU NA JAMAA WOTE WA MAREHEMU , BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE...AMEN.
Wednesday, May 11, 2011
AMBASSADORS OF CHRIST WAPATA AJALI
Waimbaji wa muziki wa injiri wa kundi la muziki wa injiri kutoka nchini Rwanda wajulikanao kama Ambassadors of christ juzi usiku wa kuamkia jana wamepata ajali mkoani Shinyanga walipokuwa wakitokea jijini Dar es salam Tanzania walikokwenda kufanya huduma inavyosemekana chanzo cha ajali hiyo ilikuwa ni mwendo kasi wa gli lao ambapo dereva wa kwaya hiyo alipofika eneo la tukio aliona loli ambalo lilikuwa limemesima njiani pasipo kuweka alama zozote za kujulisha kuwa ni bovu au la na hivyo alipo jalibu kulipit loli hilo ndipo alipokutana na roli jingine mbele yake na hiyo katika hali ya kutaka kujiokoa ili wasiweze kugongana uso kwa uso ndipo gali lao aina y coster lilipobanwa katikati na kupelekea waimbaji watatu wa kwaya hiyo wapoteze maisha na wengine sita wakivunjika mikono na miguu huku dereva wa ambassadors akipasuka kichwa pia miongoni mwa watu waliopoteza maisha ni pamoja na mtanzania fares amosi aliyekuwa akitafsiri nyimbo za ambassadors kutoka atika lugha ya kinyarwanda kuja katika lugha ya kiswa hili blog hii inapenda kutoa pole kwa wafiwa wote na ndugu wa marehemu halikadhalika na kwapenzi wote wa mziki wa injili Bwana ametoa na Bwaana ametwaa jna la Bwana lihimidiwe
Thursday, April 21, 2011
AFLEWO Gospel Singers Wanastahili Pongezi
waimbaji wa AFLEWO kenya
Wapenzi wa muziki wa Injili nchini wametoa pongezi za dhati kwa waimbaji mahiri wa muziki wa Injili wanaotambulika kama AFLEWO ambao wamejikita kwenye zaidi ya tano ikiwemo Tanzania na Kenya kuwa waimbaji hao wanaimba kwa moyo wa kumsifu na kumtukuza Mungu.
Rose mwimbaji wa AFLEWO Tanzania
Baadhi ya wapenzi hao wa muziki wa Injili wametolea mfano jinsi waimbaji hao walivyoweza kumsifu Mungu pale Diamond jubilee siku ya tarehe 15 mwezi huu ambapo kila aliyehudhuria tamasha hilo aliwapongeza waimbaji hao na kuwataka waendelee kumsifu Mungu.
Huduma ya Living water Makuti Kawe Yazua Mshangao kwa Wakristo
Apostle Onesmo Ndegi kiongozi wa huduma ya living water
Katika hali isiyotegemewa taarifa zinadai kuwa huduma ya living water makuti kawe imeandaa kile kinachoitwa mkesha siku ya tarehe 25 mwezi huu ambapo imeweka kiingilio cha shilingi 2,000 kwa wale watakaohudhuria pia watapatiwa supu ya ng'ombe. Wakiongea kwa masikitiko makubwa na blog hii baadhi ya wakristo wamehoji uhalali wa huduma hiyo kuwatoza watu kwenda kwenye mkesha wa ibada ya kusifu na kuabudu wakati wao wamepewa bure na wanapaswa kutoa bure sasa inakuwaje watoze fedha? je kwa wale ambao hawajaokoka wanawezaje kutofautisha disko na mkesha iwapo hata disko watu hutozwa fedha?.Wakristo hao wakionyesha kuwa wana uhakika na wanachokisema baadhi yao wamewataka viongozi wa huduma hiyo kuzuia jaambo hili la watu kutozwa fedha kwani halina tafsiri nzuri hasa kwa ulimwengu wa wakristo na watu wa mataifa.
MAMA TEDDY KWILASA KUUNGURUMA SINZA CHRISTIAN CENTRE
Kwa mara nyingine tena mtumishi wa Mungu mwalimu mama Teddy Kwilasa anategemea kuendesha semina kwa vijana wa jinsia zote siku ya tarehe 25 na 26 mwezi huu katika ukumbi wa Sinza christian centre. Taarifa zaidi kutoka vyanzo mbalimbali zinatanabaisha kuwa semina hiyo itakuwa inahusu mambo ya vijana hivyo ni fursa nzuri kwa vijana wa kike na kiume kuhudhuria ili kusikiliza Mungu anataka waishi namna gani ili waweze kumpendeza yeye na kujihakikishia maisha mema na ya furaha hasa ikizingatiwa kuwa dunia ya sasa imechafuka sana hivyo vijana wanapaswa kuwa macho ili wasije kukumbwa na anasa za kidunia na kumsahau Bwana Mungu wetu kwani ni dhahri kabisa tunapokuwa na vijana wanaomheshimu Mungu ni msaada mkubwa kwa taifa letu.
Sunday, April 17, 2011
Miriam Lukindo Amulika Watoto Wenye Mtindio Wa Ubongo
“AFLEWO” Africa Let’s Worship – Dar es salaam
Kwa mashabiki wa muziki wa Injili tuliopata fursa ya kuhudhuria tamasha la AFLEWO pale Diamond Jubilee tarehe 15 April mwaka huu kamwe hatutaweza kusahau jinsi waimbaji hao walivyoweza kumsifu Mungu katika roho na kweli wakidhihirisha ya kuwa ni wakati wa Afrika kuinuka na kumsifu Mungu huku tukisahau shida na mateso kwani sasa tunaye mwokozi Bwana Yesu Kristo anayetupigania.
TAMASHA LA PASAKA KUITIKISA NCHI
Alex Msama
Kama kuna vitu ambavyo wapenzi wa muziki wa Injili nchini wanavisubiria basi ni tamasha la pasaka litakaloandaliwa na Bw Alex Msama kupitia kampuni yake ya Msama promoters, kwenye tamasha hilo watakuwepo wanamuziki mbalimbali akiwemo pia malkia wa muziki wa Injili Rose Mhando
Rose Mhando
Tamasha hilo ambalo limeanza kutikisa kwenye vyombo mbalimbali nchini kabla ya hiyo tarehe 24 mwezi huu ambayo ndiyo siku ya tamasha tayari taarifa zimeshazagaa kila kona ya nchi huku zikimtaja rais wa jamhuri ya muungano mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kuwa ndiyo atakuwa mgeni rasmi.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete
Subscribe to:
Posts (Atom)