Saturday, May 21, 2011

TALAJIA KUPATA MAMBO MEMA

Mpendwa wangu wewe ambaye ni shabiki wa blog yangu tarajia kupata mambo mema na mazuri kupitia blog ya http://www.magele.blogsport.com/ siku si nyingi Mungu akubariki kila unapotembelea blog hii kikubwa zaidi ni kuniombea ili Mungu azidi kunipa vitu vizuri vya kukuelimisha wewe mpenzi msomaji wangu ili uzidi kukuwa kimwili na kiroho.

Sunday, May 15, 2011

HIVI NDIVYO MAZISHI YA WAIMBAJI WAWILI WA AMBASSADORS HUKO RWANDAYALIVYOKUWA


Waliokuwa waimbaji wa Ambassadors of Christ waliolala mauti Amosi,Philbert na Gatare Jim Ephraim

 Waimbaji wa Ambassadors wakiwa wamebeba jeneza



Mke wa Gatare Jim Ephraim akilia

Umati wa watu ndani ya Kanisa la Waadventista Wasabato Remera wakati wa ibada ya mazishi



Baba wa Gatare Jim Ephraim akizungumza


Mama wa Gatare Jim Ephraim


Ambassadors of Christ wakiimba kwenye ibada ya mazishi kanisani Remera

Kiongozi wa kanisa la Waadventista Wasabato nchini Rwanda  (mwenyemiwani) alitoa maneno ya faraja


Maneno ya mwisho yaliyosemwa na waliofariki, wakiwa safarini kurejea Kigali, Rwanda.


1. "KAZI NILIYOTAKIWA KUFANYA KATIKA KUNDI HILI, NIMEIMALIZA.IMEBAKI KWENU KUIENDELEZA-AMOSI PHARASE 



2. "NYOTE MLIO KATIKA GARI HII, LAZIMA MJUE KILA MTU ANA JUKUMU LA KUONGOZA KUNDI HILI, HATA KAMA KESHO MIMI SITAKUWEPO.-GATARE JIM " 



3. "DADA NAKUOMBA MSAMAHA, HATA KAMA WEWE NDO UMENIKOSEA, NAMI JINSI NILIVYOPOKEA, NAWEZA KUWA NIMEKUKOSEA PIA.-MANZI PHILBERT”


 Maneno yaliyoamsha ari kwa gari zima kuombana msamaha, na haikupita dk 10, ajali ikatokea!
 

Gari la Ambassadors of Christ Lililopata Ajali!


Gari ambalo walikuwa wamepanda wanamuziki wa kwaya ya Injili ya Ambassadors of Christ

POLENI SANA NDUGU ZETU MAJERUHI WA AJALI YA AMBASSADORS OF CHRIST


Mark Ndizeye akiwa hospitalini huko nchini Rwanda



>
                                                       Grace Kavara

Matukio ya Ajali iliyoleta Majonzi Kwenye Kundi la Kwaya La Ambassadors Of Christ!

Baadhi ya umati uliojitokeza kusubiria majeruhi na miili ya marehemu
Ndugu ,jamaa na marafiki wakiwa hospitali
Baadhi ya ndugu na jamaa na marafiki wakiwa nje ya hospitali
Helcopter iliyobeba majeruhi pamoja na miili ya marehemu
Helcopter hiyo iliyokuwa imebeba miili ya marehemu pamoja na majeruhi ikitua
Baadhi ya majeruhi wakishushwa kutoka kwenye helcopter
Ndugu na jamaa wakiwa nje ya hospitali
Baadhi ya ndugu na jamaa wakiwa katika hali ya majonzi na masikitiko makubwa

BLOG HII INAWAPA POLE NDUGU NA JAMAA WOTE WA MAREHEMU , BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE...AMEN.

Wednesday, May 11, 2011

AMBASSADORS OF CHRIST WAPATA AJALI

Waimbaji wa muziki wa injiri wa kundi la muziki wa injiri kutoka nchini Rwanda wajulikanao kama Ambassadors of christ juzi usiku wa kuamkia jana wamepata ajali mkoani Shinyanga walipokuwa wakitokea jijini Dar es salam Tanzania walikokwenda kufanya huduma inavyosemekana chanzo cha ajali hiyo ilikuwa ni mwendo kasi wa gli lao ambapo dereva wa kwaya hiyo alipofika eneo la tukio aliona loli ambalo lilikuwa limemesima njiani pasipo kuweka alama zozote za kujulisha kuwa ni bovu au la na hivyo alipo jalibu kulipit loli hilo ndipo alipokutana na roli jingine mbele yake na hiyo katika hali ya kutaka kujiokoa ili wasiweze kugongana uso kwa uso ndipo gali lao aina y coster lilipobanwa katikati na kupelekea waimbaji watatu wa kwaya hiyo wapoteze maisha na wengine sita wakivunjika mikono na miguu huku dereva wa ambassadors akipasuka kichwa pia miongoni mwa watu waliopoteza maisha ni pamoja na mtanzania fares amosi aliyekuwa akitafsiri nyimbo za ambassadors kutoka atika lugha ya kinyarwanda kuja katika lugha ya kiswa hili blog hii inapenda kutoa pole kwa wafiwa wote na  ndugu wa marehemu halikadhalika na kwapenzi wote wa mziki wa injili Bwana ametoa na Bwaana ametwaa jna la Bwana lihimidiwe