Thursday, April 21, 2011

AFLEWO Gospel Singers Wanastahili Pongezi

waimbaji wa AFLEWO kenya


Wapenzi wa muziki wa Injili nchini wametoa pongezi za dhati kwa waimbaji mahiri wa muziki wa Injili wanaotambulika kama AFLEWO ambao wamejikita kwenye zaidi ya tano ikiwemo Tanzania na Kenya kuwa waimbaji hao wanaimba kwa moyo wa kumsifu na kumtukuza Mungu.
Rose  mwimbaji wa AFLEWO Tanzania

Baadhi ya wapenzi hao wa muziki wa Injili wametolea mfano jinsi waimbaji hao walivyoweza kumsifu Mungu pale Diamond jubilee siku ya tarehe 15 mwezi huu ambapo kila aliyehudhuria tamasha hilo aliwapongeza waimbaji hao na kuwataka waendelee kumsifu Mungu.

Huduma ya Living water Makuti Kawe Yazua Mshangao kwa Wakristo


 
  Apostle Onesmo Ndegi kiongozi wa huduma ya living water
Katika hali isiyotegemewa taarifa zinadai kuwa huduma ya living water makuti kawe imeandaa kile kinachoitwa mkesha siku ya tarehe 25 mwezi huu ambapo imeweka kiingilio cha shilingi 2,000 kwa wale watakaohudhuria pia watapatiwa supu ya ng'ombe. Wakiongea kwa masikitiko makubwa na blog hii baadhi ya wakristo wamehoji uhalali wa huduma hiyo kuwatoza watu kwenda kwenye mkesha wa ibada ya kusifu na kuabudu wakati wao wamepewa bure na wanapaswa kutoa bure sasa inakuwaje watoze fedha? je kwa wale ambao hawajaokoka wanawezaje kutofautisha disko na mkesha iwapo hata disko watu hutozwa fedha?.Wakristo hao wakionyesha kuwa wana uhakika na wanachokisema baadhi yao wamewataka viongozi wa huduma hiyo kuzuia jaambo hili la watu kutozwa fedha kwani halina tafsiri nzuri hasa kwa ulimwengu wa wakristo na watu wa mataifa.

MAMA TEDDY KWILASA KUUNGURUMA SINZA CHRISTIAN CENTRE
















Kwa mara nyingine tena mtumishi wa Mungu mwalimu mama Teddy Kwilasa anategemea kuendesha semina kwa vijana wa jinsia zote siku ya tarehe 25 na 26 mwezi huu katika ukumbi wa Sinza christian centre. Taarifa zaidi kutoka vyanzo mbalimbali zinatanabaisha kuwa semina hiyo itakuwa inahusu mambo ya vijana hivyo ni fursa nzuri kwa vijana wa kike na kiume kuhudhuria ili kusikiliza Mungu  anataka waishi namna gani ili waweze kumpendeza yeye na kujihakikishia maisha mema na ya furaha hasa ikizingatiwa kuwa dunia ya sasa imechafuka sana hivyo vijana wanapaswa kuwa macho ili wasije kukumbwa na anasa za kidunia na kumsahau Bwana Mungu wetu kwani ni dhahri kabisa tunapokuwa na vijana wanaomheshimu Mungu ni msaada mkubwa kwa taifa letu.

Sunday, April 17, 2011

Miriam Lukindo Amulika Watoto Wenye Mtindio Wa Ubongo


Miriam Lukindo
Habari njema kwa watoto wenye mtindio wa ubongo kwani sasa Mungu ametenda miujiza kwa kumtumia mwanamuziki wa Injili Miriam Lukindo kuongoza harakati za kusaidia kundi hilo la jamii lililosahaulika kwani kuna taarifa rasmi kuwa mwimbaji huyo ambaye pia ni mke wa mwanasaikolojia Chriss Mauki ameanzisha harakati za kusaidia watoto wenye mtindio wa ubongo kupata fursa ya elimu , habari zaidi zinadai kuwa pamoja naye wanawake wengine ambao wanaunga mkono harakati hizo ni pamoja na mama Regina Lowassa, Mama Salma Kikwete, Martha Mlacha na Vicky Kamata.
Blog hii inamtakia kila la heri Miriam Lukindo kwenye nia yake hiyo njema.


“AFLEWO” Africa Let’s Worship – Dar es salaam

Kwa mashabiki wa muziki wa Injili tuliopata fursa ya kuhudhuria tamasha la AFLEWO pale Diamond Jubilee tarehe 15 April mwaka huu kamwe hatutaweza kusahau jinsi waimbaji hao walivyoweza kumsifu Mungu katika roho na kweli wakidhihirisha ya kuwa ni wakati wa Afrika kuinuka na kumsifu Mungu huku tukisahau shida na mateso kwani sasa tunaye mwokozi Bwana Yesu Kristo anayetupigania.

TAMASHA LA PASAKA KUITIKISA NCHI

Alex Msama
Kama kuna vitu ambavyo wapenzi wa muziki wa Injili nchini wanavisubiria basi ni tamasha la pasaka litakaloandaliwa na Bw Alex Msama kupitia kampuni yake ya Msama promoters, kwenye tamasha hilo watakuwepo wanamuziki mbalimbali akiwemo pia malkia wa muziki wa Injili Rose Mhando
Rose Mhando
Tamasha hilo ambalo limeanza kutikisa kwenye vyombo mbalimbali nchini kabla ya hiyo tarehe 24 mwezi huu ambayo ndiyo siku ya tamasha tayari taarifa zimeshazagaa kila kona ya nchi huku zikimtaja rais wa jamhuri ya muungano mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kuwa ndiyo atakuwa mgeni rasmi.
                                                             Rais Jakaya Mrisho Kikwete